Pages

Monday

Mapigano mengine yazuka Sudan


Siku ya Jumaane, Sudan Kusini iliteka visima vya mafuta vya eneo la Heglig, ambavyo 
vinaleta moja kati ya pato kubwa la Sudan Kaskazini.
Mapambano ya hivi karibuni, yamezusha wasiwasi kuwa vita kamili vitarudi.
Mapigano yametokea Kuek, katika jimbo la Sudan Kusini la Upper Nile, karibu na
 mpaka wa Sudan Kaskazini.
Kundi la wapiganaji linaloongozwa na Johnson Oliny, limeshambulia mji huo, 
kwa mujibu wa msemaji.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini, alisema, kwamba Kuek ilitekwa kwa 
muda mfupi, lakini ilikombolewa na wanajeshi wake.
Kanali Philip Aguer alilishutumu jeshi la Sudan kwamba liliwasaidia wapiganaji
 kwa mizinga.
Alisema Sudan Kaskazini inajaribu kuzusha vita kwengineko, kabla ya kufanya 
shambulio kubwa dhidi ya Heglig.
Haikuwezekana kupata taarifa kutoka jeshi la Sudan Kaskazini.
Kanali Aguer piya alisema wanajeshi wake katika eneo la Heglig limeshambuliwa
 kwa ndege Jumapili kutwa.

1 comment:

  1. jamani tumueke mwenyezi mungu mbele mapigano ayana maana yoyote

    ReplyDelete