Kundi la vyama vya siasa nchini Guinea Bissau limetupilia mbali
pendekezo la jeshi linalohusika na mapinduzi ya wiki hii kuunda
serikali ya mpito mpaka pale uchaguzi wa urais utakapofanyika .
Vyama hivyo vilikutana na jeshi jumanne na mazungumzo zaidi
yanatarajiwa kufanyika jumapili. Vyama vya siasa vinataka suluhisho
linalotokana na katiba ya nchi.
Jeshi lilichukua udhibiti alhamisi na kuvuruga kampeni za uchaguzi
na kutumbukiza taifa hilo la magharibi katika ghasia mpya.
Uongozi wa jeshi ulimkamata mgombea aliye mstari wa mbele
wa kiti cha urais na waziri mkuu wa zamani Carlos Gomes Junior
pamoja na rais wa mpito Raimundo Pereira na kuwatia jela baada ya
kuvamia nyumba zao.
jumuiya za kimataifa zimeshutumu vikali mapinduzi hayo ya
kijeshi katika taifa hilo la magharibi ambalo april 29 lilitarajiwa
kufanya uchaguzi wa marudio. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa
Ban ki- Moon na baraza la usalama la umoja wa mataifa walitoa
taarifa kama hiyo.
basi huo mzozo usuluishwe kwa amani
ReplyDelete