Pages

Friday

Mapigano yamemalizika Sudan na Sudan Kusini.

Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir akizungumza na televisheni ya taifa ya nchi hiyo.
Mapigano hatimaye yamemalizika kwenye mpaka wa Sudan na Sudan Kusini ambapo mashambulizi ya anga na ardhi yalifanyika wiki hii.
Mpaka Alhamisi  asubuhi vikosi viliripotiwa kuondoka kwenye pande zote za mpaka. Lakini kungali na idadi ndogo ya wanajeshi,vifaru na magari makubwa kwenye eneo la Heglig ikiwa ni ushahidi wa vita vilivyotokea.
Mapigano hayo yanamefanywa siku kadhaa kabla ya mkutano wa marais wa Sudan na Sudan Kusini uliotegemewa  kuzungumzia mafao ya mafuta na mipaka. Rais wa Sudan Omar al-Bashir amesema anasitisha mkutano huo wa Aprili 3 na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kwa sababu ya ghasia hizo.

No comments:

Post a Comment