September 11 ni siku ambayo kwa Marekani ni alama kubwa kutokana na mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa miaka 11 iliyopita, lakini september 11 2012 imekua alama kwa Nigeria baada ya mwanamke kujifungua mtoto wa farasi.
Tukio limetokea wakati mwanamke huyu akiwa kanisani kwenye maombi huko Sapele-Benin Expressway Edo state ambapo alijifungua wakati wakiwa kwenye maombi.
Mtandao wa Naijagists umeripoti kwamba mwanamke huyu kabla ya kujifungua alipiga sana kelele kama yuko kwenye chumba cha kujifungulia wakati maombi yakiendelea ambapo damu zilianza kumtoka sehemu zake za siri na baadae kujifungua huyu mtoto wa farasi ambae alifariki kabla ya waandishi wa habari kufika kwenye hilo kanisa.
Mtumishi wa Mungu aliepata nafasi ya kuzungumza baada ya hii ishu kutokea amesema wamekua wakishuhudia miujiza mingi ikifanyika kanisani kwao lakini hili la mwanamke kujifungua mtoto wa farasi ndio limetokea kwa mara ya kwanza
Hii ishu!!!! hahaha...end times with the media world!
ReplyDeletendio hivyo maajabu duniani hayo
ReplyDelete