imeandikwa na sauti ya amerika
Mahakama ya uhalifu wa kivita kwa ajili ya Rwanda imemhukumu kifungo cha
maisha jela afisa wa zamani wa Rwanda Callixte Nzabonimana kwa mauaji
ya halaiki. Mahakama hiyo ya kimataifa kwa ajli ya Rwanda ilisema
waziri huyo wa zamani alichochea mauaji ya watu kati ya 15 hadi 60 wa
kabila la Tutsi mwezi Aprili mwaka wa 1994 katika eneo la Nyabikenke.
Ilisema pia kuwa alichochea watu mara tatu hadharani mwezi huo kuwauwa
Watutsi na akaingia kwenye makubaliano ya kuwauawa watu wa kabila hilo
na serikali ya muda ya Rwanda wakati huo. Nzabonimana alikuwa waziri wa
maswala ya vijana wa Rwanda katika serikali ya muda iliyoundwa mwaka wa
1994. Alikamatwa mwezi Februari nchini Tanzania na kukabidhiwa mahakama
ya kimataifa ya uhalifu kwa ajili ya Rwanda yenye makao yake mjini
Arusha, Tanzania. Wanamgambo wa Kihutu inakisiwa waliuawa watu laki 8 wa
kabila la Tutsi na Wahutu wenye msimamo wa kadri wakati wa mauaji ya
halaiki mwaka huo wa 1994. Mahakama hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa
Mataifa ilibuniwa kwa ajili ya kusikiliza kesi dhidi ya wahusika wakuu
wa mauaji ya halaiki ya Rwanda.
No comments:
Post a Comment