imeandikwa na bbc swahili 
Kumetokea utata mpya kuhusu hisa za Facebook katika 
masoko ya hisa wiki iliyopita baada ya wasiwasi kuzuka kutokana na mauzo
 ya hisa hizo wiki iliyopita na jinsi zilizouzwa.
                     
                     
Wasimamizi wa fedha wanachunguza iwapo kiongozi 
wa mpango Morgan Stanley, aliwadokeza baadhi tu ya wateja wake kuwa 
faida ya hisa za Facebook zilizotarajiwa zimeshushwa daraja.
Morgan Stanley amekanusha hilo na kusema kuwa uuzaji wa hisa hizo ulifuata kanuni sahihi.
Bei za hisa za kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii imeshuka tangu mauzo yake kuzinduliwa rasmi kwa umma Ijumaa iliyopita.
Matatizo ya kiufundi katika siku ya kwanza ya mauzo hayo yalisababisha baadhi ya wawekezaji kupoteza fedha.
 
No comments:
Post a Comment