Na Sauti ya Amerika
Vyombo vya habari vya Marekani vinaashiria kwamba Rais Barack Obama amemshinda mpinzani wake mgombea wa chama cha Republican Gavana Mitt Romney katika uchaguzi ulokuwa na ushindani mkubwa.
Kufuatana na utaratibu wa uchaguzi wa Marekani rais anapata ushindi kutokana na idadi ya wajumbe wa majimbo na hivyo kutokana na takwimu ni kwamba Obama anapata kura 303 nae Romney anapata 206.
Ushindi wake unatokana na kushinda majimbo yaliyokuwa na ushindani mkubwa ya Ohio, Florida, na Iowa. hadi hivi sasa kura zingali zinahesabiwa na inatarajjiwa matokeo rasmi yatatangazwa baadae Jumatano.
Sherehe zimeanza katika pembe mbali mbali za Marekani hasa ngome ya chama cha Demokratic, huku Rais Obama akiwa huko Chicago, mji anakotoka akisubiriwa kutowa hotuba ya ushindi baada ya mpinzani wake Romney kutoa hotuba ya kukiri ushindi.
No comments:
Post a Comment