Chama cha Kandanda cha England (FA) kilimtia hatiani mchezaji huyo
wa kimataifa wa Serbia siku ya Jumanne baada ya picha za mkanda wa
video kuonesha akimtandika ngumi Shaun Maloney kabla Juan Mata
hajapachika bao la ushindi.
Ivanovic alipinga mashtaka hayo lakini jopo la wajumbe wa FA
likashikilia alikuwa na hatia.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 28 atakosa michezo mitatu
ijayo ya Chelsea, ukiwemo ule wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham.
FA waliweza kuchukua hatua hiyo kwa kufuata utaratibu wa
makosa yaliyopita kwa sababu mwamuzi Mike Jones na wasaidizi
wake hawakuona tukio likitendeka wakati huo.
Pamoja na mechi dhidi ya Tottenham, Ivanovic hataweza kuitetea
Chelsea wakati itakapokwenda kucheza dhidi ya Arsenal
tarehe 21 mwezi huu wa Aprili na pia siku nane baadae dhidi ya QPR.
No comments:
Post a Comment