Rais wa Sudan kusini amekataa kuondoa majeshi ambayo
yameteka mji wa mpakani ulio na mzozo na Sudan wiki hii.
Akizungumza na bunge alhamisi Salva Kiir amesema hatatoa
amri ya kujitoa kwa vikosi vya Sudan Kusini kutoka mji wa
Heglig, licha ya wito wa Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa kufanya hivyo.
Alisema pia kuwa majeshi ya sudan kusini huenda yakaingia
katika eneo lingine la mpakani lenye mgogoro, Abyei, kama
umoja wa mataifa hautalazimisha sudan kujitoa katika eneo hilo.
Uhasama kati ya Sudan na Sudan Kusini wiki hii umepelekea
wasiwasi kuwa nchi hizo zitaingia tena kwenye vita.
imeandikwa na voa.
No comments:
Post a Comment