breaking news:zaidi ya watu 30 wauwawa -Kenya(tana river).
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya limesema mapigano baina ya
makabila mawili ya ndani yanayojishughulisha na mifugo na kilimo
kusinimashariki mwa nchi hiyo yamepamba moto Jumatatu huku watu 38
wakiwa wameuwawa wakiwemo polisi tisa.
Katibu mkuu wa shirika la Msalaba mwekundu Kenya Abbas Gullet amesema
jumatatu kwamba watoto nane ni miongoni mwa waliouwawa katika shambulizi
hilo ambalo takriban watu 300 wa kabila la pokomo walivamia kijiji cha
Orma wa kabila la wafugaji. Wavamizi hao walichoma nyumba 167.
Gullet anasema ingawa makabila hayo mawili yamekuwa yakipigana mara kwa
mara kugombea ardhi na vyanzo vya maji lakini ghasia za mwaka huu
zinaweza kuwa na uchochezi wa kisiasa.
Ijumaa wajumbe 11 kutoka kabila la Pokomo waliuwawa na jumuiya ya Orma
katika tukio la kujibu mashambulizi. Watu wa kabila la Pokomo mapema
waliwauwa wajumbe 52 wa Orma.
mambo haya mpaka lini kenya?
ReplyDelete