Msemaji wa serikali anasema kundi dogo la wanamgambo liliingia
katika
jengo la ofisi ya waziri mkuu jana asubuhi wakidai malipo
kwa waliokuwa
wapiganaji waliokuwa wakimpinga Gadhafi.
Upinzani huo baade uliongezeka na kufikia watu 200, wakiwemo
wanamgambo kutoka maeneo ya milimani ya magharibi mwa nchi,
na kiasi cha
magari makubwa 50 yaliyokuwa na silaha.
Msemaji anasema baadhi ya waasi waliingia ndani ya jengo na kufyatua
risasi kutokea ndani, wakati wengine walikuwa wakifyatua risasi
wakiwa
kwenye eneo la jengo hilo.
Afisa usalama anasema waandamanaji 14 walikamatwa.
Serikali ya mpito ya Libya imetoa mishahara kwa waliokuwa
wanamgambo
ambao walipigana katika mapinduzi ya mwaka jana
yaliyomng’oa mamlaka
kiongozi wa muda mrefu wa Libya, Moammar Gadhafi.