Polisi nchini Kenya wanasema shambulizi la gruneti kwenye Kanisa
moja jijini Nairobi limeuwa mtu mmoja Jumapili na kuwajeruhi vibaya
wengine .
Polisi bado wanachunguza tukio hilo. Shambulizi la Jumapili limefanyika
Polisi bado wanachunguza tukio hilo. Shambulizi la Jumapili limefanyika
siku 6 baada ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya kuonya juu ya uwezekano
wa shambulizi la kigaidi mjini Nairobi. Ubalozi huo ulitoa ujumbe huo ukionya
raia wa Marekani kutahadhari.
Ubalozi huo ulisema una habari za kuaminika kuwa huenda mahoteli na
Ubalozi huo ulisema una habari za kuaminika kuwa huenda mahoteli na
majengo mashuhuri ya serikali mjini Nairobi yakashambuliwa na magaidi.
Aidha taarifa hiyo ya ubalozi ilisema wakati mahsusi wa shambulizi hilo
hujulikani lakini yaaminika wanaopanga shambulizi hilo wamo katika hatua
za mwishoni.