Pages

Saturday

Bunge kuishambulia Serikali kwa kukumbatia ufisadi





















Mjadala wa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za serikali katika bunge la Tanzania

uimechukua sura mpya baada ya mbunge wa kambi ya upinzani Zitto Kabwe

kukusanya saini ya asilimia 20 ya wabunge ili kuwasilisha hoja ya kupiga kura ya

kutokuwa na imani ya serikali.


Mbunge kabwe amesema katika kanuni za bunge ibara ya 123 inataka kuwepo

na asilimia hiyo ili kutoa fursa sahihi ya kuwasilisha kwa spika wa bunge kusudio

la hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.

Asilimia 20 ni sawa na wabunge 70 zoezi lililotarajiwa kufanyika kwa siku tatu .

Tayari wabunge 73 wameshatoa sahihi zao na hoja hiyo itawakilishwa kwa spika

wa bunge  bi Anne Makinda jumatatu ijayo ili aweze kuruhusu hoja hiyo ijadiliwe

bungeni ambapo inahitajika zaidi ya nusu ya wabunge ili kuweza kupitisha hoja hiyo.

Amesema sababu kubwa ya kuamua kuchukua hatua hiyo ni kutokana na ubadhilifu

na matumizi mabaya ya fedha za umma ambayo yameripotiwa na mdhibiti na mkaguzi

mkuu wa hesabu za serikali yakihusisha mawaziri watano. Waziri mkuu wa Tanzania

alitolewa mwito wa kuwafukusa kazi mawaziri hao hatua ambayo bado hajaitekeleza. 

1 comment: