Maafisa wa Marekani wanasema Marekani na China zimekubaliana kuwa msimamo wa pamoja katika swala la urushaji wa kombora wa Korea Kaskazini ambalo linatishia kuvuruga mkutano wa wiki hii wa usalama wa nyuklia huko Seoul.
Msaidizi wa rais wa Marekani Barack Obama amesema rais wa China Hu Jintao alieleza wasiwasi mkubwa wa taifa lake kuhusu mpango huo wa kurusha kombora katika mkutano baina yake na Bw. Obama Jumatatu.
Naibu mshauri wa maswala ya usalama wa kitaifa nchini Marekani Ben Rhodes aliwaelezea waandishi wa habari juu ya swala hilo kwenye mkutano . Alisema Bw. Hu alimwambia rais wa Marekani kwamba China tayari imeeleza wasiwasi wake kwa Pyongyang . Amesema viongozi hao wawili wamekubaliana juu ya hatua za kuchukua ikiwa kombora hilo litarushwa.
Katika maelezo yake Jumapili Bw.Obama amewaasa wachina kulichukulia kwa uzito ukaidi wa nyuklia wa Korea Kaskazini na kutumia ushawishi wake kuizuia Pyongyang kutengeneza . China ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini , lakini Beijing inasema ushawishi wake wa kisiasa kwa Pyongyang ni mdogo.
No comments:
Post a Comment