Wednesday
Rais Barack Obama ashinda uchaguzi Marekani
Na Sauti ya Amerika
Vyombo vya habari vya Marekani vinaashiria kwamba Rais Barack Obama amemshinda mpinzani wake mgombea wa chama cha Republican Gavana Mitt Romney katika uchaguzi ulokuwa na ushindani mkubwa.
Kufuatana na utaratibu wa uchaguzi wa Marekani rais anapata ushindi kutokana na idadi ya wajumbe wa majimbo na hivyo kutokana na takwimu ni kwamba Obama anapata kura 303 nae Romney anapata 206.
Ushindi wake unatokana na kushinda majimbo yaliyokuwa na ushindani mkubwa ya Ohio, Florida, na Iowa. hadi hivi sasa kura zingali zinahesabiwa na inatarajjiwa matokeo rasmi yatatangazwa baadae Jumatano.
Sherehe zimeanza katika pembe mbali mbali za Marekani hasa ngome ya chama cha Demokratic, huku Rais Obama akiwa huko Chicago, mji anakotoka akisubiriwa kutowa hotuba ya ushindi baada ya mpinzani wake Romney kutoa hotuba ya kukiri ushindi.
Tuesday
Mourinho kutoa uhakika wa ushindi
'Messi' wa Liverpool ni Luis Suarez
Meneja wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers,
amesema mshambulizi wa timu yake Luis Suarez anaweza kufananishwa na
Luis Suarez, kufuatia bao zuri la kupendeza mno, na la kusawazisha,
walipoikaribisha Newcastle siku ya Jumapili.
Suarez alifunga bao hilo la kusisimua mno katika uwanja wa Anfield. "Anacheza kama mchezaji nambari tisa asiyefahamika vyema yuko wapi, kama anavyofanya Messi katika klabu ya Barcelona, na anapocheza huru na wachezaji wa upinzani inabidi kumfuata nyuma kwa kasi anapojipenyeza kati yao," Rodgers aliielezea kampuni ya matangazo ya televisheni ya Sky.
Suarez hasa ndio aliisababishia timu ya upinzani matatizo makubwa, mara kwa mara akiishambulia Newcastle, na wakati mwingi akicheza katikati ya uwanja, na hata pia katika eneo la ulinzi.
Liverpool tayari walikuwa wamelemewa wakati Yohan Cabaye alipotangulia kufunga, kabla ya Suarez hatimaye kusawazisha katika kipindi cha pili.
"Tulivunjika moyo tuliposhindwa kupata ushindi," aliongeza Rodgers.
"Tulipata nafasi za kutosha kupata ushindi, lakini sina malalamiko kuhusiana na hayo.
"Mara tu tutakapoweza kupata wachezaji wa kiwango hicho na wanaoweza kufikia hadi ya mchezo wetu, basi tutakapoweza kuwika katika mechi kama hiyo tutakuwa na nafasi bora zaidi."
Wamarekani kuhitimisha upigaji kura Jumanne
Na Sauti ya Amerika
Jumanne ni siku muhimu kwa wapiga kura wa Marekani kuhitimisha zoezi la
upigaji kura katika majimbo yote ili kumpata mshindi katika uchaguzi wa
urais ulio na ushindani mkubwa.Rais wa Marekani Barack Obama na mpinzani wake Mitt Romney siku ya jumatatu walifanya kampeni za dakika za mwisho kwa wapiga kura katika majimbo muhimu ikiwa imebakia siku moja kabla ya uchaguzi katika juhudi za mwisho kuvunja ushindani.
Katika majimbo ya wisconsin , rais Obama alimshutumu bwana Romney kwa kujaribu kurejesha mawazo mabaya aliyoyatoa kabla na kusema taifa haliwezi kufanikiwa bila kuwa na daraja la kati lenye nguvu.
Kwenye mkutano wa jana asubuhi katika jimbo la kusini la Florida bwana Romney aliwaambia wafuasi wake kwamba kiongozi huyo aliyoko madarakani Mdemocrat ameshindwa kutekeleza ahadi zake wakati aliposhinda kiti cha urais mwaka 2008.
Monday
Friday
Tuesday
Obama na Romney wachuana katika mdahalo wa mwisho.
na sauti ya amerika
Rais wa Marekani Barack Obama na mpinzani wake Mitt Romney wamepambana katika mdahalo wa tatu na wa mwisho huku Bw.Obama akisema mapendekezo yote ya sera ya mambo ya nje ya Romney yamekuwa ni makosa.
Gavana huyo wa zamani wa Massachusets alijibu mashambulizi kwa rais Jumatatu usiku katika jimbo la Florida akisema kumkosoa si ajenda kwa kuzuia ghasia katika mashariki ya kati.
Bw.Romney alikosoa sera za Obama za mambo ya nje akisema ameona kurudi nyuma kwa kiasi kikubwa kwa aina ya matumaini tuliyokuwa nayo.
Bw.Obama amesema Marekani imefanya kazi kubwa na washirika wake kuleta amani na demokrasia katika eneo hilo na kuitaja Libya kama mfano.
Kuhusu Iran Obama amesema utawala wake umeonyesha uwezo kwa kuweka vikwazo vikali kuliko vyote katika nchi hiyo ya kiislam.
Subscribe to:
Posts (Atom)