Pages

Friday

shambulizi la kigaidi laepushwa na polisi


Polisi wa Kenya wanasema wameepusha shambulizi kubwa la kigaidi likiwa katika hatua za mwisho za matayarisho, na kukamata watu wawili wakiwa na milipuko, silaha na risasi.

Watu hao wawili walikamatwa katika mtaa wenye wahamiaji wengi wa Kisomali mjini Nairobi, alisema Boniface Mwaniki, mkuu wa kikosi cha kupambana na ugaidi. Alisema watu hao wanashukiwa kuwa na uhusiano na makundi ya al-Shabab la Somali linalosemekana kuwa na uhusiano na al-Qaida.


Polisi walikuta fulana nne za kujitoa mhanga, mabomu mawili, bunduki nne aina ya AK-47, risasi na mabomu 12 ya mkononi, alisema na kuongeza kuwa fulana hizo ni sawa na zile zilizotumiwa katika shambulizi la Uganda katika kundi la watu waliokuwa wakiangalia mpira mwaka 2010 na kuuwa watu 76.

No comments:

Post a Comment