Pages

Saturday

Waislam Dar es Salaam Waandamana Kulaani Filamu Iliyomkashifu Mtume


BAADHI ya waumini wa dini ya Kiislamu jana jijini Dar es Salaam wamefanya maandamano katika viwanja wa Kidongo Chekundu ikiwa ni hatua ya kuungana na Waislamu katika nchi mbalimbali kupinga filamu iliyotengenezwa nchini Marekani ikimkashfu kiongozi wao (Mtume) pamoja na dini ya Kiislamu.
 
Taarifa za awali zilieleza awali waumini hao kupitia viongozi wao waliomba kibali cha kufanya maandamano kuelekea viwanja vya Jangwani lakini walizuiwa kutokana na uwanja huo kuwa na shughuli zingine. Baada ya kuzuiwa waliamua kuandamana kwenye eneo hilo bila kibali chochote lakini hakukuwa na kikwazo chochote.
Waandamanaji walionekana wameshika mabango yaliokuwa na ujumbe wa kuyalaani mataifa ya Marekani na Israel huku wakiitaka Serikali kufuta ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kutokana na filamu wanayoilalamikia kutengenezwa katika taifa hilo.
 
  
 
                                                  picha na thehabari 

No comments:

Post a Comment