Proscovia Alengot Oromait wa nchini Uganda ameweka rekodi barani
Afrika kwakuwa mbunge mwenye umri mdogo kuliko wote kwa kuingia mjengoni
akiwa na miaka 19 tu.
Kama unadhani aliupata kwa viti maalum, futa wazo hilo kwakuwa
msichana huyo ameshinda kwenye uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge
kilichokuwa kikikaliwa na baba yake.
Awali Oromait alikuwa amepanga kwenda chuo lakini aliamua kuingia
kwenye siasa baada ya kifo cha baba yake Michael Oromait mwezi July,
aliyekuwa mbunge wa jimbo la Usuk lililopo mashariki mwa Uganda.
Akiwa na miaka hiyo, Oromait aliwagalagaza wagombea watu wazima
wanane ambapo alimzidi kura mara mbili mgombea aliyekuwa nyuma yake.
Shirika la habari la Associated Press limedai kuwa kuchaguliwa kwake kuna faida kwa chama tawala cha rais Yoweri Museveni.Oromait amekuwa mbunge wa pili mwenye umri mdogo duniani.
No comments:
Post a Comment