Kufuatia mjadala mkali bungeni kuhusu matumizi mabaya ya fedha na
juhudi za kutaka kuwasilisha hoja ya kutokua na imani na Waziri Mkuu,
Rais Kikwete ameiarifu kamati kuu ya chama tawala cha CCM katika
kikao
cha dharura kwamba atafanya mabadiliko katika baraza lake la
mawaziri.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye amesema kwamba,
"kamati kuu imepokea kwa furaha na kwa kweli
imeridhia na kubariki
uwamuzi wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, kulisuka upya
baraza la mawaziri, na kuwawajibisha mawaziri
kwa mujibu wa jinsi
walivyohusika na kuhusishwa kwenye zile taarifa."