Viongozi hao wameamua kuunda jopo litalokwenda Sudan Kusini
kutathmini ikiwa nchi hiyo inatimiza vile vipengele vinavyofaa kabla
ya kukubaliwa kuwa mwanachama.
bado watu wanamashaka kama Sudan Kusini inafaa kukubaliwa kwenye
jumuia wakati iko vitani na Sudan.
kuna maoni tofauti - kuna wale wanaofikiri Sudan Kusini inaweza
kusaidiwa kumaliza mgogoro wake na Sudan endapo imo ndani ya jumuia.
Wengine wanaona afadhali kusubiri hadi vita vitulie.
Lakini kwa sasa ombi la Sudan Kusini linaangaliwa kwa makini, anasema
mwandishi wetu.
Sudan iliwahi kuomba kujiunga na Jumuia ya Afrika Mashariki lakini ilikataliwa.