Pages

Thursday

Jeshi la SPLA laondoka kwenye mpaka wa Sudan


Child soldiers of the rebel Sudan People's Liberation Army (SPLA) wait for their commander at a demobilization ceremony at their barracks in Malou, southern Sudan Sunday, February 25, 2001 (file photo).


Sudan kusini imeondoa majeshi yake katika eneo linalogombaniwa kwenye mpaka wa Sudan kufuatia mapigano ya wiki hii na majeshi ya Sudan. Mapigano hayo mapya yamerudisha nyuma juhudi za kutatua mzozo kati ya nchi hizo mbili. 

Naibu waziri wa ulinzi wa Sudan kusini Majak D’ Agoot amesema jeshi linalojulikana kama SPLA limejiondoa katika mji unaogombaniwa wa Heglig.

Wanajeshi wa SPLA walipigana na majeshi ya sudan katika eneo hilo kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanyika sudan kusini katika jimbo la unity mapema wiki hii. Khartoum imekanusha tuhuma hizo na imeishutumu Juba kwa kuchochea mapigano.

D’Agoot ameiambia sauti ya amerika kuwa wanajeshi wa SPLA waliondoka Heglig jumanne na sasa wanafanya doria kusini mwa mpaka.

Anasema hatua hiyo ilikuwa ni juhudi ya kupunguza mivutano na kuruhusu kurejea kwa  mashauriano  na Khartoum ambayo yanasimamiwa   na umoja wa afrika .

Khartoum na Juba zimekuwa katika mazungumzo mjini Addis Ababa kutatua masuala kadhaa  ambayo bado hayajatatuliwa wakati Sudan Kusini ilipojitangazia uhuru kutoka Kaskazini mwezi Julai mwaka jana kufuatia miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. 

Moja ya ajenga ya juu ni  mzozo wa mafuta. Sudan kusini ilifunga vinu vyake vya uzalishaji mafuta  mwezi januari baada ya kuishutumu Sudan kuiba mafuta yanayopitia katika mabomba ya kaskazini. 

No comments:

Post a Comment