Pages

Friday

sagna "nina shaka na arsenal"

  Mlinzi wa Arsenal, Bacary Sagna, na ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa, ameelezea wasiwasi kuhusiana na mipango ya usajili ya klabu. Timu ya The Gunners imemruhusu Robin van Persie na Alexander Song kuondoka msimu huu wa joto, na mwaka jana iliwaachia wachezaji Cesc Fabregas, Samir Nasri na Gael Clichy kuondoka. 
 
 Nilitazamia Robin kuondoka," alisema Sagna,"Lakini nilishangazwa na kuondoka Alex. Ana umri wa miaka 24, na alikuwa na miaka mitatu iliyosalia katika mkataba wake.Sagna alijiunga na Arsenal kutoka klabu ya Auxerre mwezi Julai mwaka 2007, na ameichezea Arsenal mechi 205.


Hivi sasa amepumzishwa, kwani bado anaendelea kupona baada ya kuvunjwa mguu katika mechi dhidi ya Norwich mwezi Mei. 



Mkataba wake utakwisha mwisho wa msimu wa mwaka 2013-14, na alipoulizwa kama kuna yeyote ambaye ameshauriana naye kuhusiana na mkataba mpya, alisema "La, hakuna yeyote aliyezungumza nami."

 

No comments:

Post a Comment