Pages

Friday

Rais Barack Obama amekubali rasmi kuwa mgombea kiti cha rais kwa niaba ya chama cha Demokratik


Rais Barack Obama amekubali rasmi kuwa mgombea kiti cha rais kwa niaba ya chama cha Demokratik katika hotuba yake Alhamisi, aliyowahimiza wafuasi wake kuungana pamoja nae kaika awamu ya mwisho ya miezi miwili ya kampeni za kupigania kiti cha rais Marekani.

Ilikuwa hotuba yake muhimu kabisa kaika kampeni, na Wademoktrats walimpongeza kwa shangwa kubwa mjini Charlotte, alipotetea juhudi zake za kuokoa uchumi wa nchi hii, na kuwaomba wamrudhishe kwa awamu ya pili White House.

 
 "Wamarekani na mtambuwe kitu kimoja, maatizo yetu yanaweza kutanzuliwa. Changamoto zetu zinaweza kutanzuliwa. Hivyo njia tunayopendekeza huwenda ikawa ngumu zaidi, lakini inatuongoza katika mahala bora zaidi. Na nina waomba muchaguwe mustakbal huo," alisema.
 

No comments:

Post a Comment