Pages

Thursday

Rais mpya wa somalia anusulika kufa na shambulio la bomu



rais mpya wa somalia
Miripuko miwili ya bomu imetikisa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu Jumatano nje ya hoteli ya Al Jazeera ambako rais mpya wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Kenya Sam Ongeri walikuwa wanakutana na waandishi habari.

Rais Mohamud na waziri Ongeri hawakujeruhiwa. Inaripotiwa kulikuwepo na ujumbe mkubwa wa Wakenya wakiwemo wabunge walofuatana na waziri Ongeri pamoja na wajumbe wa mashirika ya kimataifa mjini Mogadishu Waziri mkuu wa Somalia aneondoka Abdiweli Mo0hamed Ali alikua pia ndani ya hoteli wakati wa shambulio hilo.mwili wa mjitoa mhanga mmoja ulikuwa nje ya mlango wa hoteli na mwili wa mjitoa mhanga mwengine ulikuwa karibu na hoteli ndani ya gari


Takriban watu watano wameuwawa wakiwemo wanajeshi wa AMISOMO walokuwa wanalinda hoteli hiyo, na inasemekana huwenda idadi hiyo ikaongezeka.

 

No comments:

Post a Comment