Pages

Wednesday

Wanamgambo wavamia ofisi ya waziri mkuu libya




Msemaji wa serikali anasema kundi dogo la wanamgambo liliingia
 katika jengo la ofisi ya waziri mkuu jana asubuhi wakidai malipo 
kwa waliokuwa wapiganaji waliokuwa wakimpinga Gadhafi.
Upinzani huo baade uliongezeka na kufikia watu 200, wakiwemo
 wanamgambo kutoka maeneo ya milimani ya magharibi mwa nchi,

 na kiasi cha magari makubwa 50 yaliyokuwa na silaha.
Msemaji anasema baadhi ya waasi waliingia ndani ya jengo na kufyatua
 risasi  kutokea ndani, wakati wengine walikuwa wakifyatua risasi 
wakiwa kwenye eneo la jengo hilo.
Afisa usalama anasema waandamanaji 14 walikamatwa.
Serikali ya mpito ya Libya imetoa mishahara kwa waliokuwa 
wanamgambo ambao walipigana katika mapinduzi ya mwaka jana 
yaliyomng’oa mamlaka kiongozi wa muda mrefu wa Libya, Moammar Gadhafi.