imeandikwa na DW
Mtoto wa Afrika akiwa ndani ya maji kwenye chombo cha kumuongeshea
Mtoto Ayabo Rose
Hosipitali ya La Genera ACCRA-Ghana ambacho ni kituo cha kwanza kutoa
chanjo. Wanaonekana akina mama wakiwa na watoto wao migongoni wakijongea
kupata chanjo katika foleni maalumu kila mmoja wao anaiheshimu foleni
inayowapa nafasi ya kupata matone ya chanjo.
Mandhari ya eneo hilo ikipambwa na kilio cha mtoto akijua kuwa sasa anaenda kudungwa sindano kumbe anafuata matone ya chanjo.

Wakipatiwa msaada na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshugulikia
watoto, UNICEF, kwa sasa kati ya watoto wadogo chini ya miaka mitano
1000 watoto 80 wanaofariki chini ya umiri huo wakati kwenye mataifa
mengine barani humo hali inatisha, mfano katika Somalia kati ya watoto
1000 watoto180 wanafariki kabla ya kufiki umri wa miaka mitano.
Mafanikio yakiwa makubwa kwa mataifa ya Ulaya, Sweden na Finland kati
ya watoto1000 ni watoto watatu tu ndiyo wanaofariki chini ya umri huo.
Ghana imeshauriwa kupunguza kabisa vifo vya watoto kutoka 80 hadi 40.
Kwa sasa chanjo wanazopatiwa watoto hao ni pamoja na Virusi vya Rota na
Pneumococcal kwa ajili ya homa ya mapafu.
Wakati chanjo zikiendelea kutolewa asimilia 87 ya chanjo za Polio,
Kifua Kikuu, Pepopunda, Homa ya manjano na chanjo nyingine za watoto
zimetolewa.
Akiwa kazini, mhudumu wa afya ndani ya nyumba moja akitoa chanjo, hapa anataja umuhimu wa chanjo ya polio.
"Chanjo ya polio tunawapa watoto kujikinga na ugonjwa huu ambapo
wakipata ugonjwa huo hatari mwili unapoooza, ila ukimpa chanjo mapema
inazuia kabisa kuambukizwa ugonjwa huo." anasema mhudumu wa Afya.
Chanjo hizo wanapewa watoto kabla ya kufikia miezi minne ambapo vituo
vya Afya kadhaa vimepewa chanjo, wengine wakizunguka majumbani
kuhakikisha watoto wote wanafikiwa na mpango huo, lakini changamoto
kubwa ni kuzishawishi baadhi ya kaya ambazo wanaamini kuwa kumpa chanjo
mtoto kuna madhara hasa wale wanaoamini katika ushirikina.
Taasisi ya muunganiko wa GAVI imefanikisha kuwafikia watoto 400,000
katika taifa hili lenye watu milioni 25. Huku chanjo hizo zinategemea
kupunguza vifo vya homa ya manjano kwa watoto 12,000, kuhara kwa watoto
10,000 wakilenga kufikia malengo ya milenia mwaka 2015 sasa wako katika
hatua nzuri.
Changamoto nyingine ni vifo vinayotokana na Malaria na Utapia mlo; hii
linanonekana wazi kuwa utapia mlo mara nyingi umekuwa ukiongeza idadi
vya vifo vya watoto hao.
Sasa kila mwanamke mjamzoto wa Ghana anaona umuhimu wa kupatiwa chanjo
kwa watoto wake. "Nikijifungua mtoto wangu salama nitampeleka kupata
chanjo." alisema mwanamke mjamzito.

Akinamama wanaojifungua wameshauriwa kuwanyonyesha watoto wao kwa miezi
sita ya mwanzo kwa kuwapa maziwa ya mama tu. Huku kukiwa na ushahidi
kuwa akina mama wengi hawafanyi hivyo kwa kutoona umuhimu wa kunyonyesha
watoto na wengine wakibanwa na majukumu ya kazi katika sekta
mbalimbali.
Mwandishi:Adeladius Makwega
No comments:
Post a Comment