Pages

Monday

Mauaji ya kikatili nchini Syria


                              imeandikwa na sauti ya amerika
Serikali ya Syria inalaumu  kile inachoita magaidi waliokuwa na silaha kwa mauaji ya kikatili ya zaidi ya raia 108 siku ya  Ijumaa karibu na mji wa Homs. Lakini mashahidi wengi wanasisitiza kuwa vikosi vinavyounga  mkono serikali ndivyo  vilifanya mauaji hayo ya kikatili. Maandamano yenye jazba juu ya mauaji ya raia yaliyofanyika  Ijumaa huko Houla yanaendelea kote nchini Syria hiyo jana, ikiwa ni pamoja na mji mkuu Damascus  ambako vikosi vya uslama vilishambulia kwa risasi waandamanaji katika mtaa wa Midan. Msemaji wa wizara ya masuala ya nchi za nje wa Syria Jihad Makdissi aliwaambia waandishi habari kuwa jeshi la Syria halina lawama  juu ya  shambulizi la Ijumaa akisema wakulaumiwa ni magaidi waliokuw ana silaha. Mashambulizi hayo yalifanywa kwa saa  tisa ambapo pamoja na mauaji, nyumba zilichomwa moto na mali kupora.

No comments:

Post a Comment