Pages

Wednesday

Gavana wa zamani Nigeria Jela miaka 13








 

 

 

 

James Ibori, gavana wa jimbo la Delta alikiri kujihusisha na makosa 10 ya
 ulaghai na biashara ya fedha haramu.
Mahakama ya Southwark Crown ilielezwa kuwa kiasi cha fedha alichoiba kutoka
 kwa watu wa jimbo la Delta kilikuwa ‘hakihesabiki’".
Ibori, aliyeepuka kukamatwa Nigeria baada ya kundi la mashabiki wake kuvamia
 kituo cha polisi, alikamatwa Dubai mwaka 2010.
Alihukumiwa Uingereza ambako alishtakiwa kwa ushahidi uliotolewa
na Polisi wa London.
Mojawapo ya mashtaka yake Ibori alikiri kuhusika na udanganyifu wa kiasi
cha $37m (£23m) kuhusu mauzo ya hisa za jimbo la Delta kwa kampuni ya
 simu nchini Nigeria iliyobinafsishwa ya V Mobile.
Alikuwa gavana wa Jimbo la Delta kati ya Mei 1999 na Mei 2007.
Wakili wa upande wa mashataka Sasha Wass, aliiambia mahakama kuwa
 Ibori "kwa makusudi na kwa mpangilio " aliwalaghai watu waliomchagua
 kuwawakilisha.
Mahakama pia iliarifiwa kuwa alikuja Uingereza miaka ya 1980 na kufanya
 kazi kama mhasibu wa duka la Wickes DIY huko Ruislip, kaskazini magharibi mwa
London.

 Kuinuka na kuanguka kwa James Ibori

1958: Alizaliwa Jimbo la Delta, Polisi wa Uinegereza wanaamini.
1980: Alihamia Uingereza
1991: Alishtakiwa kwa kuliibia duka la DIY, Wickes
1992: Alihukumiwa kwa udanganyifu
1993-4: Alijihusisha mwenyewe na utawala wa kijeshi waNigeriawa Sani Abacha
1999: Alichaguliwa gavana wa Jimbo la Delta
2007: Alijiuzulu kuwa gavana
2007: Uingereza ilitia tanjimaliyenye thamani ya $35m
Desemba 2007: Alikamatwa na mahakama ya Nigeria kwa tuhuma za rushwa.
2009: Mahakama ya Nigeria ilimfutia mashtaka
April 2010: Mashabiki wa Ibori walivamia kituo cha polisi wakijaribu kumkamata
Mei 2010: Alikamatwa Dubai
2011: Alihamishiwa Uingereza
2012: Alifungwa London
Alishtakiwa mwaka 1991 akiiba kwenye duka lakini alirejeshwa Nigeria na alianza
 kupanda kisiasa mpaka kwenye mtandao wa chama cha People's Democratic (PDP)
Alipowania ugavana alidanganya tarehe yake ya kuzaliwa kuficha uhalifu aliotuhumiwa
 kufanya Uingereza ambao ungemzuia kugombea nafasi hiyo.
Ibori, ambaye anwani yake ilitolewa kuwa ni Primrose Hill, Kaskazini mwa London,
 anadai kuwa na miaka 53 lakini polisi wa London wanasema ana miaka 49.
James Ibori
Alikuwa gavana mwaka 1999 lakini alianza kuchukua fedha za hazina za jimbo.

Alinunua:

 
·         Malikatika eneo la Shaftesbury,Dorset, kwa £311,000
·         Jumba la kifahari la kiasi cha £3.2m huko Sandton, karibu na Johannesburg,                                Afrika Kusini.
·         Gari ya kifahari lenye uwezo wa kuhimili mashambulio ya silaha aina
          ya zote[Range Rovers] yenye thamani ya £600,000
·         Gari aina ya Bentley £120,000
·         Gari aina ya Mercedes Maybach kwa Euro 407,000 ambayo ilisafirishwa
          kwenda katika jumba lake la kifahari Afrika Kusini


Baada ya kusikiliza kesi hiyo, Sue Patten, mkuu wa kitengo cha mashtaka
 alisema mahakama itaomba mali zake zitaifishwe na kurejesha utajiri alioupata
 ‘kwa gharama ya baadhi ya watu maskini kabisa duniani’
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa Andrew Mitchell alisema: ‘Hukumu ya
James Ibori inatoa ujumbe mzito na wa muhimu kwa wale wanaotaka kutumia
Uingereza kuficha uhalifu wao wakiwa kama wakimbizi’
"Ufisadi ni saratani katika nchi zinazoendelea na serikali ya muungano haitavumilia hali hiyo."
Jumatatu kipindi cha BBC Newsnight kilionyesha kuwa mfuko wa misaada
 wa kitengo cha Uingereza cha maendeleo ya Kimataifa kinachoshughulikia
miradi CDC Group, ukichunguzwa na maafisa wa Nigeria.
Kilifichua madai yanayoashiria kuwa CDC Group liliweka $47.5m (£29.9m)
 katika mfuko binafsi yaliyowekeza Nigeria yakituhumiwa kuhusishwa na Ibori.
DfID lilisema tuhuma hizo zilikuwa za mwaka 2009 na CDC, ambayo inayosimamiwa
 na Bw Mitchell, siku zote imekuwa ikifanya "uchunguzi wa makini " kabla ya kuwekeza
 kwenye mfuko huo.
CDC ilichunguza madai hayo wakati huo, na kukuta ‘hakuna dalili kuwa mfuko
 huo wa Uingereza umetumika vibaya", alisema.
           NIMENUKUU HABARI HII TOKA BBC

1 comment: