Pages

Thursday

AU yaanza kumsaka Joseph Kony


Maafisa wa jeshi la Uganda wanasema jeshi la Uganda linalomsaka kiongozi wa waasi Joseph Kony wamekabidhi uongozi wa operesheni hizo kwa majeshi ya Umoja wa Afrika kutoka Uganda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kulingana na Meja Alex Ahabyona wa Uganda sherehe hizo zilifanyika Jumanne katika mji wa Nzara, Sudan Kusini. Kikosi hicho cha AU, ambacho kilitangazwa mapema mwaka huu, kilishindwa kuanza kazi mapema kutokana na kukosa vifaa na wanajeshi. Haijafahamika kati ya wanajeshi 5,000 waliotakiwa ni wangapi wakipatikana mpaka sasa lakini kufanyika kwa sherehe hiyo ni ishara kuwa wanajeshi wa kutosha wamepatikana. Kikosi hicho cha AU kitafanya kazi chini ya kamanda wa Kiganda Kanali Dick Olum. Wanajeshi 100 wa Marekani wanasaidia serikali za eneo hilo katika juhudi za kumsaka na kumwangamiza Kony na kundi lake katili la LRA

No comments:

Post a Comment