Wananchi wa Misri wanapiga kura katika siku ya pili na ya mwisho ya uchaguzi wa rais kupata kiongozi mpya baada ya kutimuliwa kwa Hosni Mubarak mwaka jana.
Wapiga kura wanachagua baina ya mgombea kutoka enzi za Mubarak – waziri mkuu wa zamani Ahmed Shafiq – na mgombea wa chama cha kiislamu Muslim Brotherhood, Mohammed Morsi.
Utokezaji wa wapiga kura jumamosi ulikuwa sio mzuri sana na hali haikuonyesha hamasa kama ilivyokuwa katika raundi ya kwanza ya uchaguzi mwezi uliopita. Mwandishi wa Sauti ya Amerika mashariki ya kati anaripoti kuwa huenda wapiga kura wamekatishwa tamaa na tofauti kubwa za kisera zilizopo kati ya wagombea. Mgombea mmoja aliyekuwa na sera za kadiri aliondolewa