Pages

Friday

China yasababisha tembo kupungua Afrika




















Kuongezeka kwa idadi ya tembo wanaouliwa barani Afrika kunahusishwa na kuongezeka mahitaji  ya pembe nchini China kulingana na taasisi ya kimataifa ya masuala ya wanyama.

Ripoti inasema kuwa mwaka 2011 majangili  walikusanya zaidi ya meno ya tembo 5,200 au tani 23, na kusababisha vifo vya zaidi ya tembo 2,500. Inasema pembe nyingi zilipelekwa  China.

Meneja mawasiliano Elizabeth Wamba anafanya kazi na mfuko wa fedha wa kimataifa wa masuala ya wanyama katika Afrika mashariki. “Kukua  kwa mahitaji ya bidhaa za  pembe za ndovu nchini China,  kumechangia  uwindaji  haramu wa tembo kote Afrika. Umekuwa juu mno. Umeongezeka katika  sehemu kadhaa, kwa asilimia 100”.

Ripoti hiyo inakariri jarida  moja la mnada likielezea mauzo  ya mwaka 2011 ya zaidi ya vipande 11,000 vya pembe za ndovu   nchini  China kwa jumla ya dola milioni 95.4  ongezeko la asilimia 107 kutoka mwaka mmoja uliopita.

Ripoti inasema bei ya pembe imeongezeka  lakini  kuimarika kwa  sarafu ya China dhidi ya dola ya Marekani kumefanya iwe na faida kubwa kwa  wanunuzi wa China kununua pembe kwenye masoko ya dunia.


Ripoti hiyo inaelezea ongezeko la mahitaji  kwa mauzo halali  ya shehena ya pembe  nchini China na Japan mwaka 2008. Shehena hiyo  ilitokea  Afrika kusini, Zimbabwe, Namibia na Botswana.

Televisheni ya serikali ya China iliripoti kwamba wawekezaji wa kawaida wanaziangalia bidhaa za  pembe za ndovu kama “dhahabu nyeupe”.

Ripoti inasema China ilianzisha  mwaka 2004 mfumo wa kudhibiti  soko la ndani la pembe kwenye mkutano wa kimataifa wa biashara kuhusu wanyama waliohatarini kutoweka,  lakini hakuna kanuni zinazofuatwa.

Kati ya viwanda vya biashara 158 vya pembe  vilivyofanyiwa utafiti na wataalamu wa China katika miji mitano, 101 vilikuwa vikifanya kazi kinyume cha sheria, havikuwa na leseni yeyote iliyotolewa na serikali.

                              imeandikwa na sauti ya amerika

No comments:

Post a Comment