imeandikwa na sauti ya amerika
Serikali ya Syria inalaumu kile inachoita magaidi waliokuwa na silaha
kwa mauaji ya kikatili ya zaidi ya raia 108 siku ya Ijumaa karibu na
mji wa Homs. Lakini mashahidi wengi wanasisitiza kuwa vikosi vinavyounga
mkono serikali ndivyo vilifanya mauaji hayo ya kikatili. Maandamano
yenye jazba juu ya mauaji ya raia yaliyofanyika Ijumaa huko Houla
yanaendelea kote nchini Syria hiyo jana, ikiwa ni pamoja na mji mkuu
Damascus ambako vikosi vya uslama vilishambulia kwa risasi waandamanaji
katika mtaa wa Midan. Msemaji wa wizara ya masuala ya nchi za nje wa
Syria Jihad Makdissi aliwaambia waandishi habari kuwa jeshi la Syria
halina lawama juu ya shambulizi la Ijumaa akisema wakulaumiwa ni
magaidi waliokuw ana silaha. Mashambulizi hayo yalifanywa kwa saa tisa
ambapo pamoja na mauaji, nyumba zilichomwa moto na mali kupora.
No comments:
Post a Comment