Pages

Monday

Ajali ya ndege ya Nigeria yauwa abiria wote

Wananchi wakirusha mabaki ya ndege ya Dana Airlines , katika eneo la makazi ya watu kaskazini mwa uwanja wa ndege wa   kimataifa wa Murtala Muhammed Jumapili Juni 3, 2012.
 Maafisa wa Nigeria wanasema abiria  wote 153 waliokuwa kwenye ndege. wamefariki dunia baada ya ndege hiyo kuangukia jengo  la makazi mjini  Lagos. Rais wa nigeria(  Goodluck Jonathan )ametangaza siku 3 za maombolezo ya kitaifa kwa ajili ya waathirika na kuamuru uchunguzi wa kina kufanyika juu ya janga hilo. Maafisa kutoka idara ya anga ya Nigeria wamesema ndege ya Dana Airlines ilikuwa ikisafiri Jumapili kutoka Abuja kwenda Lagos  ilipoangukia jengo la ghorofa mbili kwenye eneo la makazi ya watu wengi na kusababisha majengo mengine kuungua. Yaaminika abiria wote  153 kwenye ndege hiyo wamefariki dunia. Haikujulikana mara moja ikiwa  kuna mtu yeyote  ardhini aliyeuawa. Shirika la ndege  la Dana lina ndege nyingi  aina ya Boeing MD-83 ambazo husafirisha abiria kwa saa nzima kutoka Abuja kwenda Lagos.

1 comment: