Pages

Tuesday

INTERNATIONAL NEWS: njama za Alqaeda za zuiwa, Ndege iko salama



                                           makala hii imeandikwa na sauti ya amerika


Maafisa wa Marekani wanasema wamezuia njama za ulipuaji bomu 
za alqaeda zilizolenga kulipua ndege iliyokuwa ikisafiri kuja Marekani .
Maafisa hapa Marekani wanasema  tawi la alqaeda huko Yemen
 lilidhamiria kumweka mlipua mabomu wa kujitoa muhanga kwenye
 ndege iliyokuwa ikielekea  Marekani,  milipuko ilikuwa imefungwa
 kwenye nguo za ndani za mlipuaji huyo.
Wanasema njama hizo ziligunduliwa na bomu hilo kukamatwa kabla
 ndege yeyote kuingia hatarini.
Baraza la  taifa la usalama la White House limesema kwenye taarifa 
yake jumatatu kuwa rais wa Marekani Barack Obama alipewa taarifa 
kwanza  kuhusu njama  hizo  mwezi Aprili na kupata taarifa za kila 
wakati kuhusu hali hiyo. Ilisema rais alihakikishiwa kwamba chombo
 hicho hakileti hatari kwa umma.